Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 13:46

Maandamano yenye ghasia yameingia siku ya tatu Charlotte


Ofisa polisi akijaribu kumshika muandamanaji huko Charlotte, North Carolina-NC.
Ofisa polisi akijaribu kumshika muandamanaji huko Charlotte, North Carolina-NC.

Mkuu wa polisi katika mji wa Charlotte katika jimbo la North Carolina nchini Marekani alisema hana mpango wa kutoa video ya ufyatuaji risasi iliyosababisha kifo cha mwanamme mweusi aliyeuwawa na maafisa polisi licha ya siku tatu za maandamano.

Ghasia zilizuka katika mji mkubwa huko North Carolina baada ya ufyatuaji risasi uliopelekea kifo cha Keith Lamont Scott mwenye umri wa miaka 43 wakati alipokuwa akitoka nje ya gari lake siku ya Jumanne.

Polisi wa mji wa Charlotte huko North Carolina
Polisi wa mji wa Charlotte huko North Carolina

Polisi wanasema alikuwa na bunduki lakini familia yake inasema hakuwa na bunduki na huwenda alikuwa amebeba kitabu cha kujisomea. Alhamis jioni iliingia siku ya tatu ya maandamano yanayodai kutolewa kwa mkanda wa video wa tukio hilo pamoja na wito wa kumaliza ukiukaji unaofanywa na polisi dhidi ya wamarekani weusi.

Baadhi ya waandamanaji walivaa vitambaa vinavyofunika pua zao wakijihadhari iwapo polisi watatumia gesi ya kutoa machozi ambapo walishika mabango yakisomeka “Know Justice, Know Peace” The People versus the State” na “stop Killing Us”.

XS
SM
MD
LG