Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 10:28

Maandamano yapangwa Malawi


Polisi wa kupambana na ghasia Malawi
Polisi wa kupambana na ghasia Malawi

Rais Bingu wa Mutharika aonya juu ya maandamano ya Jumatano

Rais wa Malawi Bingu wa Mutharika ametoa mwito kwa wanaharakati kufutilia mbali maandamano ya kupinga serikali yaliyopangwa kufanyika Jumatano.Makundi ya kutetea haki za kiraia yanapanga kile yanachoita makundi ya uangalizi ya kijamii kupinga kile wanachosema ni kushindwa kwa serikali kushughulikia matakwa yao. Akizungumza kupitia televisheni ya kitaifa Jumapili, rais Mutharika alinasema huenda hali Jumatano ikageuka kuwa ya ghasia.Amewaomba waandalizi wa maandamano hayo kutafakari upya juu ya hatua hiyo. Mwezi jana watu 19 waliuawa baada ya kuzozana na polisi katika maandamano ya kupinga serikali yaliyofanywa katika miji mitatu ya Malawi. Maandamano hayo yamechochewa na ufukara unaokithiri katika kila pembe ya nchi, uhaba wa mafuta na fedha za kigeni. Rais Mutharika ameapa kuendelea kuwakamata viongozi wa maandamano ya mwezi Julai. Ijumaa iliyopita waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague alieleza wasiwasi wake juu ya hali nchini Malawi. Alimwomba rais Mutharika kuruhusu “mjadala halali wa kidemokrasia” na kuzungumza na makundi ya kutetea haki za kiraia. Uingereza ilidhibiti msaada kwa Malawi mapema mwaka huu kufuatia mzozo wa kidplomasia.

XS
SM
MD
LG