Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 27, 2023 Local time: 17:43

Maandamano yaongezeka Ufaransa, baada ya Rais Macron kusaini sheria yenye utata kuhusu pensheni


Maandamano ya kupinga mpango wa pensheni wa Rais Macron, Paris, Machi 15, 2023

Waandamanaji walifunga barabara kuu karibu na mji mkuu wa Ufaransa na kuzidisha mgomo katika vituo vya kusafisha mafuta leo Ijumaa kudhihirisha kwa mara nyingine hasira yao baada ya Rais Emmanuel Macron kupitisha mageuzi yenye utata kuhusu pensheni bila kura ya wabunge.

Hatua ya Macron ilichochea maandamano nchini kote Alhamisi usiku, huku watu 300 wakikamatwa nchi nzima, kwa mujibu wa waziri wa mambo ya ndani.

Leo asubuhi, waandamanaji wapatao 200 wamezuia kwa muda usafiri wa barabarani kwenye barabara kuu nje ya mji mkuu Paris.

Katika sekta ya nishati, waandamanaji wanatarajiwa kusitisha uzalishaji kwenye kituo kikuu cha kusafisha mafuta mwishoni mwa juma au Jumatatu, mwakilishi wa chama cha wafanyakazi wa sekta hiyo Eric Sellini amesema.

Alhamisi, rais alitumia mamlaka yake ya kikatiba yenye utata kwa kupitisha sheria ya pensheni kwa amri ya kiutendaji, hali ambayo ilichochea maandamano nje ya bunge mjini Paris kadhalika katika miji mingine kadhaa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG