Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 26, 2023 Local time: 06:29

Maandamano yanaendelea Misri licha ya onyo la wanajeshi


Maandamano yanaendelea Misri licha ya onyo la wanajeshi

Waandamanaji walienedelea kukusanyika Cairo Jumapili kudai kuundwa serikali ya mseto licha ya wanajeshi kutaka mivutano ya kisiasa kumalizika.

Siku moja kabla ya uchaguzi wa bunge kuanza Jumatatu huko Misri, maelfu ya waandamanaji walishuka tena katika uwanja wa Tahrir, mjini Cairo na kuendelea kudai kuundwa kwa serikali ya mseto ya kiraia na kuwataka wanajeshi kuacha madarala mara moja.

Mtawala mkuu wa kijeshi Jemedari Mkuu Hussein Tantawi ameonya kwamba kutakuwepo na athari mbaya ikiwa mvutano wa kisiasa wa hivi sasa nchini humo hautamalizika mara moja.

Tantawi pia amesema baraza la utawala la kijeshi halita waruhusu waharibifu kuvuruga uchaguzi wa bunge ulopangwa kuanza Jumatatu.

Alisema nchi iko katika njia panda na inaweza kuchagua njia ya uchaguzi wenye matokeo itakayoiongoza Misri kuelekea usalama au kukabiliwa na vizingiti vya hatari ambavyo jeshi halitaruhusu.

XS
SM
MD
LG