Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 01, 2023 Local time: 07:19

Maandamano yakumba Ecuador


Polisi waasi wa Ecuador.
Polisi waasi wa Ecuador.

Ecuador imetangaza hali ya dharura baada ya Polisi na Wanajeshi kuingia mitaani kupinga kupunguzwa kwa matumizi kadhaa ya bajeti

Ecuador imetangaza hali ya dharura baada ya Polisi na Wanajeshi kuingia mitaani kupinga kupunguzwa kwa matumizi kadhaa ya bajeti na kurusha mabomu ya kutoa machozi kwa rais Rafael Correa.

Bw.Correa alikuwa akikutana na waandamanaji nje ya kituo cha Polisi huko Quito wakati baadhi ya waandamanaji walipoanza kumshambulia. Kopo la bomu la kutoa machozi lilirushwa kutoka kwa waandamanaji na kutua karibu na rais.

Rais huyo aliwapa changamoto washambuliaji hao kumuuwa kabla ya wasaidizi wake kumwondoa na kumpeleka hospitali ambapo aliwashutumu waandamanaji hao kwa kufanya jaribio la kutaka kupindua serikali yake.

Akizungumza akiwa bado hospitali bwana Correa alisema polisi waasi bado wanajaribu kuingia katika hospitali anakotibiwa kupitia paa la jengo hilo.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton anasema Marekani inashutumu vikali ghasia hizo na kwamba Marekani inamuunga mkono Rais Correa na demokrasia nchini Ecuador.

XS
SM
MD
LG