Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 07, 2024 Local time: 01:02

Maandamano yaitishwa Saudia Ijumaa


Maandamano Saudi Arabia
Maandamano Saudi Arabia

'Siku ya hasira' imetangazwa nchini Saudi Arabia Ijumaa kupinga utawala wa kifalme

Wanaharakati nchini Saudi Arabia wanatumia mtandao wa internet kuwasihi raia nchini humo kuingia mitaani Ijumaa kwa maandamano ya hadhara ya kupinga serikali katika kile wanachoita ‘Siku ya Hasira’ .

Mwito huo umetolewa licha ya marufuku iliyowekwa na serikali dhidi ya kufanya maandamano kama hayo baada ya mwito uliotolewa mapema mwezi huu kwa raia wa Saudia kuandamana. Serikali ilichukua hatua hiyo baada ya makundi madogo ya waandamanaji kukusanyika yakidai mabadiliko katika utwala wa kifalme nchini humo.

Mikutano mikubwa ya upinzani ni nadra huko Saudia, lakini maelfu ya watu wameungana kupitia mtandao wa internet wakiitisha maandamano mjini Riyadh Ijumaa wanayosema yatatumiwa kushinikiza mabadiliko ya kisiasa na kijamii nchini humo.

Mnamo mwezi Februari, mfalme Abdullah alitangaza baadhi ya mageuzi katika juhudi zinazoonekana kuwarai raia wasiingie katika maandamano yanayotawala nchi nyingi za Mashariki ya kati .

XS
SM
MD
LG