Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 12:14

Maandamano yaitishwa Angola


Maafisa wa ulinzi Angola
Maafisa wa ulinzi Angola

Maandamano ya kupinga rais wa Angola yapangwa kufanyika Jumatatu

Maelfu ya raia wa Angola wamefanya maandamano ya amani kuunga mkono rais Jose Eduardo dos Santos.Maandamano hayo ya kuunga mkono serikali yamefanyika katika mji mkuu Luanda, siku moja kabla ya maandamano yaliyopangwa kufanywa Jumatatu dhidi ya serikali hiyo,na ambayo yametangazwa na watu wasiojitambulisha kupitia mtandao wa internet.

Maafisa wa Angola wakizungumza kupitia vyombo rasmi vya habari,wameonya raia dhidi ya kuhudhuria maandamano hayo Jumatatu. Hakuna chama cha upinzani kilichojitokeza kuunga mkono maandamano hayo.

Rais Santos ameongoza nchi hiyo tangu mwaka wa 1979. Angola ina utajiri mkubwa wa almasi na mafuta lakini raia wake wanaishi katika ufukara na miundombinu yake ni mbovu kufuatia vita vya miaka 27 vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika mwaka wa 2002.

XS
SM
MD
LG