Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 15:58

Maandamano makubwa yaendelea katika nchi za Kiarabu


Waandamanaji wanachana bendera ya Marekani waloivuta kutoka ubalozi wa Marekani Cairo. Sept11, 2012.

Maandamano makubwa yanafanyika katika nchi za kislamu kulaani filamu inayomkejeli Mtume Mohamed iliyotengenezwa hapa Marekani.Polisi wamepambana na waandamanaji Khartoum, sanaa

Maandamano yamenedelea kwa siku ya nne mfululizo katika nchi za kislamu kote duniani kulalamika filamu inayomkejeli Mtume Mohamed na kudhalilisha dini ya kislamu.

Waandamanaji wamevamia afisi za ubalozi za Ujerumani na Uingereza, mjini Khartoum wakati polisi walipambana na waandamanaji nje ya ubalozi wa Marekani mjini Cairo. Polisi walifyetua mabomu ya kutowa machozi kutawanya waandamanji mjini Khartoum, Cairo na Sanaa.

Maelfu ya waandamanaji walivamia mgahawa wa kimarekani wa kuuza kuku Kentucky Fried Chicken katika mji wa Tripoli Lebanon na kulitia moto jengo na baadhi ya wafanyakazi wamefariki.

Akizungumza na Sauti ya Amerika, mhadhir wa chuo kikuu cha Al-Azhar mjini Cairo Ismael Mfaoume anasema waandamanaji walikusanyika pia katika uwanja wa Tahrir wakiitaka serikali kuvunja uhusiano na Marekani.

please wait

No media source currently available

0:00 0:06:00 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Serikali mbali mbali za dunia zimeimarisha usalama katika afisi za ubalozi za nchi za Magharibi pamoja na afisi za mashirika ya misaada. Waandamanaji wamekuwa wakitia moto bendera za Marekani na Israel katika miji kadhaa ya nchi za kislamu.

XS
SM
MD
LG