Wakristo waliandamana wakibeba misalaba iliyotengenezwa kwa mbao na kupaaza sauti na kutoa ujumbe kwa lugha ya kiarabu unaosema kwamba wao ni wanajeshi wa Yesu, na kwamba kwa damu na roho, watajitolea kwa niaba ya Yesu.
Maandamano yanajiri wakati kuna ongezeko la mashambulizi dhidi ya sehemu za ibada za wakristo.
Watu wasiojulikana wakiwa na bunduki walifyatua risasi Desemba 18, dhidi ya kanisa la Orthodox mjini Hama. walijaribu pia kuharibu msalaba uliowekwa mbele ya kanisa hilo na makaburi.
Viongozi wa kanisa nchini Syria wamewashauri wakristo kupunguza sherehe za krismasi mwaka huu, licha ya ahadi kutoka kwa kwa viongozi wapya wenye kufuata itikadi kali za kislamu nchini humo kwamba kila mtu ana uhuru wa kuabudu kulingana na dini yake.
Forum