Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 10:57

Upinzani wa DRC untaendelea na maandamano kumpinga Kabila


Supporters of Democratic Republic of Congo's opposition Presidential candidate Moise Katumbi.
Supporters of Democratic Republic of Congo's opposition Presidential candidate Moise Katumbi.

Maadamano ya umma yamepigwa marufuku katika maeneo fulani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hayo ni kwa mujibu wa maafisa wa serikali.

Hatua hiyo imejiri siku moja tu kabla ya mkutano ulioitishwa na makundi ya upinzani kupinga uamuzi wa mahakama uliozua utata kwa kumruhusu Rais Joseph Kabila kuendelea kuwa madarakani.

Maandamano yamepigwa marufuku katika mashariki mwa mkoa wa Kivu Kaskazini na mji wa Lubumbashi baada ya muungano huo wa upinzani kuitisha maandamano nchini kote, kufuatia uamuzi huo wa mahakama ya maswala ya katiba, kumtaka Rais Kabila kuendelea kuwa mamlakani kama kiongozi wa muda, baada ya muhula wake kumalizika mwezi Decemba mwaka huu.

Shirika la habari la AFP limemnukuu gavana wa jimbo la Kivu ya kaskazini, akisema kuwa maandamano hayatakubaliwa kwenye mkoa huo.

XS
SM
MD
LG