Waandamanaji wanaodai uhuru wamekusanyika kote syria ijumaa ikiwemo mji mkuu Damascus na mji wa kusini ambo umekuwa ni kituo cha maandamano ya kupinga utawala wa chama cha baath.
Katika mji wa Daraa karibu na mpaka na Jordan mamia ya watu walitembea kwa kile waandaaji walichokiita “ siku ya utu’ .
Vyombo vya habari vinasema hakukua na ulinzi ulionekana katika mitaa ambako takriban watu 15 walikufa katika maandamano ya wiki hii.
Takriban watu 200 waliandamana mjini Damascus baada ya sala ya ijumaa kuwaunga mkono watu wa Daraa.
Shirika la habari la Reuters linaripoti kukamatwa kwa dazani ya watu.
Serikali ya Syria ilisema alhamisi itafikiria kuondoa sheria ya hali ya dharura nchini kama sehemu ya mlolongo wa mageuzi.
Maandamano ya kudai uhuru yazuka Syria
- Mary Mgawe

Waandamanaji wanaodai uhuru wamekusanyika kote syria ijumaa ikiwemo mji mkuu Damascus