Maandamano yatafanyika chini ya sheria kali ambazo hazijawahi kushuhudiwa, ikiwa ni pamoja na kuvaa beji yenye nambari shingoni mwa waandamanaji.
Kanuni zilizowekwa na polisi, ambao walielezea sababu za usalama, zinafanyakazi wakati kitovu cha kifedha kipo katika harakati za kurejea kwake katika hali ya kawaida baada ya Covid-19 na hali ya kisiasa.
Wakati wa janga hilo, maandamano yalifanyika kwa nadra kwa sababu ya vizuizi vya COVID-19 vilivyowekwa.
Aidha, wanaharakati wengi wamenyamazishwa au kufungwa jela baada ya Beijing kuweka sheria ya usalama wa taifa kufuatia maandamano makubwa mwaka 2019.
Wakosoaji wanasema uhuru wa kukusanyika wa eneo hilo ambao uliahidiwa wakati Hong Kong iliporejeshwa China kutoka Uingereza mwaka 1997 umemomonyoka.