Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 21:18

ZANU-PF kinasema wazimbabwe wanampenda Mugabe


Wafuasi wa chama cha upinzani wakiandamana mjini Harare, Zimbabwe wakimtaka Rais Robert Mugabe ajiuzulu.
Wafuasi wa chama cha upinzani wakiandamana mjini Harare, Zimbabwe wakimtaka Rais Robert Mugabe ajiuzulu.

Chama tawala nchini Zimbabwe kimetupilia mbali wito kutoka upinzani kwamba Rais Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 92 ajiuzulu, siku moja baada ya maandamano makubwa ya upinzani kufanyika katika muda wa miaka kadhaa.

Msemaji wa chama cha ZANU-PF, Simon Khaya Moyo, ameliambia gazeti linalomilikiwa na serikali la Herald kwamba Rais Mugabe alishinda wadhifa wake kidemokrasia na amesema wafuasi wa upinzani wanatakiwa kupiga kura ya kumuondoa madarakani badala ya kutoa wito kwa Rais kujiuzulu.

Moyo alisema kama watu bado wanamuhitaji Mugabe, watampigia kura kwa mara nyingine mwaka 2018, wakati ambapo Mugabe anatarajiwa kuwania tena nafasi hiyo.

Zaidi ya wafuasi 2,000 wa chama cha MDC-T, kinachoongozwa na Morgan Tsvangirai, waliandamana katika mitaa ya Harare jana Alhamis, wengi wao wakiwa na mavazi mekundu wakiunga mkono upinzani.

XS
SM
MD
LG