Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 09, 2022 Local time: 08:22

Maandamano ya kila Ijumaa yaendelea Misri


Waandamanaji wakipaza sauti kupinga hali ngumu ya maisha chini ya utawala wa Rais Abdel Fattah al Sisi, Cairo, Misri, Sept. 21, 2019.

Misri mapema Ijumaa imeshuhudia maandamano ya pili yanayofanyika kila mwishoni mwa wiki (Ijumaa) kulalamikia hali ngumu ya kiuchumi pamoja na ufisadi kwenye ngazi za juu za serikali.

Maandamano hayo yameonekana kukaidi marufuku iliyowekwa dhidi ya maandamano nchini humo licha ya misako inayoendelea kufanywa na vyombo vya serikali.

Msimamo mkali ulionyeshwa wiki iliyopita na Rais Abdel Fattah al Sisi baada ya kutolewa video dhidi ya utawala wake na mfanyabiashara aliyetoroka nchini Mohamed Aly umetisha waangalizi wengi kwenye taifa hilo ambalo ni maarufu katika kukandamiza kila aina ya upinzani.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG