Kifo cha Abdullah Morsi aliyefariki Jumatano ikiwa ni takribani miezi miwili na nusu baada ya baba yake kufariki kutokana na sababu zinazofanana, kulingana na maelezo ya kaka yake, pamoja na familia walipozungumza na shirika la habari la Reuters.
Taarifa kutoka familia hiyo zinaeleza Abdallah Morsi mwenye umri wa miaka 24 alianza kuhisi mshituko wa mishipa mwilini mwake wakati alipokuwa akiendesha gari mjini Cairo, huko Misri, akiwa na rafiki yake.
Baba yao alikuwa kiongozi wa kwanza kuchaguliwa kwa njia ya kidemokrasia nchini Misri. Mohamed Morsi alifariki mwezi Juni 2019 kutokana na mshtuko wa moyo akiwa na umri wa miaka 67 baada ya kuanguka akiwa ndani ya mahakama moja mjini Cairo wakati akitoa ushahidi kuhusiana na kesi ya uhaini dhidi yake.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.