Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:21

Maandamano kupinga tume ya uchaguzi Kenya


Wafuasi wa upinzani wakichoma magari na kuziba barabara wakati wa maandamano mjini Kisumu, magharibi mwa Kenya. Januari 31. 2008
Wafuasi wa upinzani wakichoma magari na kuziba barabara wakati wa maandamano mjini Kisumu, magharibi mwa Kenya. Januari 31. 2008

Maandamano ya upinzani huko nchini kenya kupinga tume ya uchaguzi nchini humo yanatarajiwa sasa kuelekezwa mjini Mombasa, kenya Jumatatu asubuhi.

Maandamano hayo yanatarajiwa kuongozwa na naibu kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha ODM bwana Ali Hassan Joho ambaye pia ni gavana wa kaunti ya Mombasa.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Sauti ya Amerika-VOA mjini Mombasa, viongozi wa upinzani walisema kwamba maandamano hayo yatakuwa ya amani kuelekea ofisi za tume ya uchaguzi huko pwani na pia wameomba jeshi la polisi kuwapatia ulinzi.

Wakati huo huo wafuasi wa muungano wa vyama vya upinzani-CORD wataandaa maandamano katika mji mkuu wa Nairobi.

XS
SM
MD
LG