Mapema Jumanne waandamanaji waliwashinda nguvu polisi na kuingia kwa nguvu kwenye majengo ya bunge na muda mfupi baadaye moshi mkubwa ulitanda katika majengo hayo.
Wabunge walitoroka kupitia njia ya chini kwa chini kutoka majengo ya bunge, lakini waandamanaji waliwaruhusu wapinzani ambao waliupinga mswaada huo kutoka nje ya jengo lililozingirwa.
Ofisi ya gavana wa Nairobi, na mjumbe wa chama cha tawala pia ilionekana ikiwaka moto.
Ghasia zilipokua zinaendelea waandishi wa habari wanasema waliona maiti ya watu watatu nje ya jengo ambako polisi walifyatua risasi.
Waandamanaji waliwataka wabunge kutoupigia kura mswaada huo wenye utata unaoongeza kodi katika nchi hiyo ambayo wananchi wake wana hasira kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha kwa miaka mingi.
Baadhi ya taarifa hii inatoka shirika la habari la AP
Forum