“Makubaliano yamefikiwa kuondoa muswada huo,” Razzaz amesema wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya kukutana na wabunge.
Mfalme Abdullah alimteua Razzaz, mmoja wa mawaziri, kama waziri mkuu mpya Jumanne baada ya Hani Mulki kujiuzulu Jumatatu wakati maandamano makubwa yakifanyika kupinga kuunga mkono kwake hatua za kubana matumizi.
Maelfu ya wananchi wa Jordan walijitokeza mitaani wakidai serikali iachilie mbali mageuzi ya kiuchumi yasiokubalika na wengi yanayotokana na sera za Shirika la Fedha Duniani (IMF) ambayo yameharibu hali za maisha ya watu.
Madaktari, mawakili na waalimu walifanya mgomo nchi nzima Jumatano, wakiwa wamekerwa na hali ya kukosekana ajira, umaskini na kuongezeka kwa bei za vitu.
Jordan imekuwa ikilaumu hali mbaya ya uchumi wake kuwa ina sababishwa na kukosekana utulivu katika eneo na jukumu kubwa la kuwaweka maelfu ya wakimbizi wa Syria bila ya kupata msaada wakutosha kutoka katika jumuiya ya kimataifa
Wakopeshaji wa kimataifa wameshinikiza kuweko mageuzi hayo ya kiuchumi kuisaidia Jordan kupunguza deni lake, kutokana na kuzorota kwa uchumi kunafungamanishwa na migogoro katika eneo.