Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 04, 2022 Local time: 02:16

Idadi ya vifo yaongezeka Baghdad


Waandamanji mjini Baghdad Iraq

Polisi na watoa huduma za afya mjini Baghdad Iraq, imeeleza kuwa idadi ya watu waliouwawa kutokana na maandamano yalokuwa yakiendelea kwa mda wa wiki moja huko mjini Baghdad Iraq sasa imefikia 110.

Wizara ya mambo ya ndani ya Iraq imeeleza kuwa zaidi ya watu elfu sita wamejurihiwa. Ghasia zilizuka kwanza katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad October mosi, pale waandamanaji walipoandamana dhidi ya ukosefu wa kazi, ukosefu wa huduma msingi na rushwa za kisiasa.

Serikali imekubali kufanya mageuzi kadhaa, ikiwa ni pamoja na kutoa ruzuku katika bodi za nyumba, misaada ya pesa kwa watu wasiokuwa na kazi na mafunzo ya kazi kwa vijana.

Hata hivyo, waandamanji wanadai mabadiliko makubwa zaidi yanahitajika, wakisema kuwa, rushwa imekithiri mno nchini humo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG