Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 11:29

Maandamano Burundi.


Waandamanaji kutoka vyama vya upinzani waandamana mjini Bujumbura, Burundi.
Waandamanaji kutoka vyama vya upinzani waandamana mjini Bujumbura, Burundi.

Waandamanaji nchini Burundi Jumanne wameendelea na maandamano na kukabiliana na polisi kwa siku ya tatu wakipinga juhudi za rais wa nchi hiyo za kushikilia uongozi kwa muhula mwingine.

Takriban watu watano wamekufa baada ya ghasia kuzuka tangu Jumapili,baada ya chama tawala cha CNDD-FDD, ambacho kimetajwa kuwakandamiza wapinzani wake, kumteua Rais Pierre Nkurunziza kama mgombea wake kwenye uchaguzi wa rais unaotarajiwa kufanyika Juni 26.

Mwanahabari wa Shirika la Habari la Ufaransa, AFP amesema kumekuwa na maafisa wengi wanaoshika doria kwenye mji mkuu Bujumbura huku mamia ya waandamanaji wakitawanywa na kuzuiliwa kuingia kwenye mji.

Rais Nkurunziza aliekuwa kiongozi wa waasi wakati mmoja, amekuwa madarakani tangu 2005. Viongozi wa upinzani pamoja na vikundi vya kutetea haki za binadamu wanasema juhudi za rais za kushikilia uongozi zinakiuka katiba na pia mkataba uliositisha mapigano ya 2006.

Maelfu ya raiya waliuwawa kwenye mapigano ya miaka 13, na kumekuwa na hofu kwamba hali ilioko ya kisiasa, huenda ikatumbukiza nchi hiyo kwenye mapigano tena.

XS
SM
MD
LG