Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 21:46

Maambukizi ya Covid-19 yapita milioni 2 Korea Kaskazini


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akiwa amevalia barakoa kwenye picha ya awali
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akiwa amevalia barakoa kwenye picha ya awali

Korea kaskazini imesema Ijumaa kwamba imeanza kupata matokeo mazuri kwenye vita dhidi ya mlipuko wa Covid 19 huku idadi ya watu waliodhibitishwa kuambukizwa ikipita milioni 2.

Wimbi la maambukizi ambalo taifa hilo lilidhibitisha kwa mara ya kwanza wiki iliyopita limezua hali ya wasi wasi kutokana na uhaba wa huduma za matibabu pamoja na chanjo,wakati likiwa limetengwa na ulimwengu pamoja na kuwekewa vikwazo vingi kutokana na kuendesha program ya nyuklia.

Afisa mmoja wa Korea kusini amesema kwamba taifa hilo bado halijajibu ombi la kupewa misaada kutoka kwa mahasimu wake Marekani na korea kusini. Rais mpya wa Korea kusini Yoon Suk Yeol, na mwenzake wa Marekani Joe Biden ambaye amewasili korea kusini mapema Ijumaa, wanatarajiwa kuzungumzia maambukizi yanayoshuhudiwa Korea kaskazini. Alhamisi taifa hilo limetangaza maambukizi mapya 263,370 na vifo viwili zaidi na kwa hivyo kufikisha jumla ya watu walioambukizwa kufika milioni 2.24 tangu mwishoni mwa Aprili.

XS
SM
MD
LG