Mlipuko wa Ebola uligunduliwa Uganda kuanzia mwezi Septemba. Ulianzania katika wilaya tatu zilizo eneo la kati kabla ya kusambaa na kuripotiwa Kampala, mji wenye zaidi ya watu milioni 1.6.
Mtu wa kwanza kuripotiwa kuambukizwa Ebola jijini Kampala, alikuwa mwanamme aliyesafiri kutoka wilaya ya Kassanda, kutafuta matibabu katika hospitali kuu ya Mulago. Mtu huyo alifariki dunia.
Wagonjwa saba kati ya tisa waliogunduliwa kuugua Ebola, wanatoka familia moja, iliyompeta mmoja wao kutoka mtaa wa Masanafu, karibu na Kampala.
Waziri wa Afya wa Uganda Jane Ruth Aceng, amesema wkamba muuguzi aliyekuwa anamtibu mwanamme huyo na mkewe, naye alifariki dunia.
Wizara ya afya ya Uganda imetoa wito kwa watu nchini humo kuwa makini sana na kutafuta matibabu iwapo wamekaribiana na mtu au familia yamtu ambaye amerithibitsihwa kuugua Ebola.
Watu 90 wamethibitishwa kuambukizwa Ebola, aina ya Sudan, nchini Uganda tangu mwezi Septemba. Watu 44 wamefariki dunia.
Virusi vya Ebola aina ya Sudan, havina chanjo.