Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 27, 2025 Local time: 05:32

Maambukizi ya Corona yaongezeka China


watu wakinunua bidhaa katika duka la jumla mjini Beijing ambao mamlaka wanataka shughuli za kawaida kusitishwa. April 25 2022 PICHA: REUTERS
watu wakinunua bidhaa katika duka la jumla mjini Beijing ambao mamlaka wanataka shughuli za kawaida kusitishwa. April 25 2022 PICHA: REUTERS

Maafisa wa afya katika mji wa Beijing, China, wameanza kupima virusi vya Corona kwa wakaazi milioni 21, kutokana na wasiwasi kuwamba huenda mji huo mkuu ukawekwa chini ya amri kali za kusitisha shughuli za kawaida kama ilivyo katika mji wa Shanghai, ili kudhibithi virusi hivyo.

Upimaji unaendelea katika wilaya 11 baada ya shughuli hiyo kuzinduliwa katika wilaya ya Chaoyang, Jumatatu.

Wakaazi wa Beijing wamesema kwamba wanaunga mkono hatu ahiyo ya serikali ili kudhibithi maambukizi ya virusi vya Corona.

Maafisa wamewasihi wakaazi katika baadhi ya sehemu za Beijing kufanyia kazi nyumbani. Baadhi ya sehemu za wazi kama zile za kufanyia mazoezi zimeanza kufungwa.

Visa 70 vya maambukizi ya virusi vya Corona vimeripotiwa tangu wiki iliyopita, ikiwemo visa 33 vilivyoripotiwa hiii leo.

Vifo vya watu 51 kati ya visa 10,000 vya maambukizi ya virusi vya Corona vimeripotiwa katika mji wa Shanghai wenye jumla ya watu milioni 26, ambao shughuli za kawaida zimefungwa.

XS
SM
MD
LG