Haya yanajiri wakati tayari maambukizi mapya yakiwa yametangazwa kwenye majimbo yenye watu wengi zaidi nchini humo, ya New South Wales na Victoria.
Takwimu rasmi zimeonyesha kwamba katika wiki ya mwisho ya Oktoba, visa vya mambukizi ya Covid-19 viliongezeka kwenye majimbo yote ya Australia isipokuwa Queensland.
Maambukizi mapya 9,707 yalitangawa kufikia mwishoni mwa wiki iliyomalizika Oktoba 29, kwenye jimbo la New South Wales pekee, likiwa ongezeko la asilimia 11 ikilinganishwa na wiki iliyotangulia.
Takwimu za serikali zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 95 ya wakazi wa taifa hilo waliyo juu ya umri wa miaka 16, tayari wamepatiwa walau dozi mbili za covid.
Kupitia video iliyowekwa kwenye mtandao wa twitter, afisa mkuu wa afya wa jimbo la New South Wales, Kerry Chant ameonya kuhusu ongezeko la maambukizi mapya.