Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 06:25

Maafisa wanne wa polisi wauawa Ufaransa


Polisi walinda doria baada ya shambulizi la kisu lililowauwa maafisa wanne wa polisi, Alhamisi Octoba 3, 2019.(AP Photo/Kamil Zihnioglu)
Polisi walinda doria baada ya shambulizi la kisu lililowauwa maafisa wanne wa polisi, Alhamisi Octoba 3, 2019.(AP Photo/Kamil Zihnioglu)

Maafisa wanne wa polisi wa Ufaransa Alhamisi waliuawa kwa kushambuliwa na kisu ndani ya makao makuu ya polisi Paris, afisa wa umoja wa polisi amesema.

Afisa huyo, Loic Travers, amesema mtu aliyewashambulia polisi hao aliuawa kwa kupigwa risasi na afisa mwengine wa polisi

Travers amesema mshambuliaji huyo inaaminika kuwa alikuwa ni mfanyakazi katika ofisi hiyo ya makao makuu, lakini hilo linasubiriwa kuthibitishwa.

Travers amesema shambulio hilo linaelekea kuwa lilianza katika ofisi moja na kuendelea kutokea katika maeneo mengine lenye uwanja mkubwa.

Meya Anne Hidalgo amethibitisha “watu kadhaa” kuwa wameuawa.

Hakuna tamko lolote lililotolewa juu ya sababu iliyopelekea shambulio hilo, lililotokea katikati ya Jiji la Paris karibu na Kanisa la Notre-Dame.

Travers amesema, hata hivyo, mshukiwa huyo aliyefanya shambulizi hilo hajawahi kuleta tatizo lolote katika eneo hilo la kazi.

XS
SM
MD
LG