Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 08:03

Mshukiwa wa mashambulizi ya Ubelgiji asakwa


Picha iliyotolewa na polisi kuhusu mshukiwa wa mashambulizi ya ubelgiji
Picha iliyotolewa na polisi kuhusu mshukiwa wa mashambulizi ya ubelgiji

Polisi wanaendelea kusaka mtu wa tatu alieonekana kwenye uwanja wa ndege akitembea pamoja na Khalid na Najim Laachraoui ambao walijiuwa wakati wa shambulizi katika uwanja huo wa Zaventem.

Maafisa wa usalama wa Brussels wanaendelea kumsaka mshukiwa mwingine aliyehusika na shambulizi la Jumanne kwenye uwanja wa ndege na kituo cha treni karibu na makao makuu ya Umoja wa Ulaya.

Mshukiwa huyo inasadikiwa kuwa alionekana kwenye kanda ya video akiwa amebeba mkoba karibu na Khalid el Bakaoui mlipuaji wa kujitoa mhanga alietekeleza shambulizi kwenye kituo cha treni cha Maelbeek. Polisi wanaendelea kusaka mtu wa tatu alieonekana kwenye uwanja wa ndege akitembea pamoja na Khalid na Najim Laachraoui ambao walijiuwa wakati wa shambulizi katika uwanja huo wa Zaventem.

Maafisa wa kijasusi wamesema kuwa Laachraoui mwenye umri wa miaka 25 alikuwa mtaalam wa kutengeneza mabomu kwenye kundi la Islamic State na kwamba alihusika na shambulizi la kigaidi mjini Paris mwezi Novemba mwaka jana.

XS
SM
MD
LG