Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 02:10

Maafisa waandamizi wazidi kuliasi jeshi la Congo


Wanajeshi wa Congo wakisubiri kupelekwa kwenye mstari wa mbele wa mapigano huko mashariki ya nchi
Wanajeshi wa Congo wakisubiri kupelekwa kwenye mstari wa mbele wa mapigano huko mashariki ya nchi

Umoja wa Mataifa unasema hali katika jimbo la Kivu ya Kaskazini inaendelea kuwa ya wasi wasi, hasa kwa vile maafisa wa jeshi wanajiunga na waasi wa M23.

Kundi la M23 limeundwa na wanachama wa zamani wa kundi jingine la waasi la CNDP lililojiunga na jeshi la serikali miaka mitatu iliyopita kufuatia makubaliano ya amani ya Goma..

Lakini wengi kati ya wapiganaji hao walianza kuliasi jeshi mwanzoni mwa mwezi wa April ili kumunga mkono kiongozi wa zamani wa waasi Bosco Ntaganda, anaesakwa kwa ajili ya uhalifu wa vita.

Mwezi May jeshi la Congo lilifanikiwa kuwarudisha nyuma wapiganaji wa M23 hadi kufikia mpaka wa Rwanda na Uganda. Lakini kufuatia tuhuma za mwezi Juni kwamba waasi hao wanapata msaada kutoka Rwanda, kasi na nguvu za mashambulizi ya jeshi ziliathirika sana na mambo kubadilika.

Msemaji wa jeshi la Umoja wa Mataifa Congo, Kanali Felix Basse anasema uwasi huo umekuwa pigo mara mbili kwa jeshi la Congo linalojulikana kama FARDC.

"Kwanza uwasi huo umedhoifisha nguvu za FARDC, na pili umekuwa na athari katika nidhamu na mori wa wanajeshi."

Kwa upande mwengine Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha Jumatano kuongeza muda wa MONUSCO huko Congo kwa mwaka mmoja na kutaka kukomeshwa mara mmoja msaada wa kutoka nje kwa waasi.

XS
SM
MD
LG