Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 19:23

Maafisa wa Ukraine waamuru kuhamishwa kwa lazima kwa karibu raia 12,000


Aftermath of a Russian missile attack in Zaporizhzhia

Naibu waziri wa Ulinzi wa Ukraine Hanna Maliar alisema siku moja kabla kwamba nguvu ya mapigano na makombora ya adui ni ya juu katika eneo hilo.

Maafisa wa Ukraine wameamuru kuhamishwa kwa lazima kwa karibu raia 12,000 kutoka miji na vijiji 37 katika wilaya ya Kupiansk ya mkoa wa Kharkiv mashariki mwa Ukraine.

Hapo ndipo majeshi ya Russia yanaripotiwa kufanya juhudi kubwa kushambulia kupitia mstari wa mbele. Utawala wa kijeshi wa eneo hilo ulielezea agizo la uhamishaji la Alhamisi kama la lazima lakini wakasema watu wanaweza kubaki ikiwa watatia saini hati inayosema watafanya hivyo kwa hiari yao bila kujali kitakachotokea.

Naibu waziri wa Ulinzi wa Ukraine Hanna Maliar alisema siku moja kabla kwamba nguvu ya mapigano na makombora ya adui ni ya juu katika eneo hilo. Wakati Ukraine ikiendeleza mashambulizi ya polepole katika wiki za hivi karibuni vikosi vya Russia vimefanya mashambulizi ya kisasi katika baadhi ya maeneo.

Forum

XS
SM
MD
LG