Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 12:20

Maafisa wa Tanzania wawekewa vikwazo vya visa na Marekani


Polisi wa kupambana na ghasia Zanzibar wanawazuia raia kwenye mtaa wa Stone Town
Polisi wa kupambana na ghasia Zanzibar wanawazuia raia kwenye mtaa wa Stone Town

Serikali Marekani leo imetangaza masharti ya visa kwa maafisa wa serikali ya Tanzania kwa kudhoofisha utaratibu wa kidemokrasia na ukiukaji wa haki za binadamu nchini humo.

Waziri wa Mambo ya Nje, Mike Pompeo katika taarifa yake amesema kuwa maafisa wa Tanzania waliohusika au kushiriki katika kudumaza uchaguzi mkuu wa taifa hilo la Afrika Mashariki wa Oktoba 28 mwaka 2020 na kuvuruga utaratibu mzima wa uchaguzi na kudhoofisha demokrasia watahusika katika masharti hayo.

“Marekani inasisitiza kwamba hatua za leo hazielekezwi kwa watu wa Tanzania. Tunawapongeza watanzania ambao walishiriki katika uchaguzi kwa amani na nia njema, na tutafanya kazi na wote wenye nia ya dhati katika kusukuma mbele demokrasia, haki za binadamu na ustawi wa pamoja, “ taarifa imesema.

Taarifa imeeleza kuwa wasimamizi wa uchaguzi na jamii za kiraia walielezea kusambaa kwa dosari pamoja na ukiukaji wa haki za binadamu kabla na baada ya uchaguzi. Wagombea wa upinzani walienguliwa kuwania nafasi, walinyanyaswa na kukamatwa.

Nchi ilishuhudia. Kusambaa kwa dosari ikiwemop kukosekana kwa huduma za internet, waandishi wa habari kunyanyaswa, na ghasia ambazo zimefanywa na vikosi vya usalama na kuufanya uchaguzi kutokuwa huru wala wa haki, taarifa imesema na kuongezea kuwa viongozi wa jamii za kiraia wanatishiwa hata baada ya ucahguzi, na viongozi wa kisiasa wakikimbia nchini kwa kukhofia usalama wao katika nchini.

Hatua maafisa wa Tanzania zilivuruga utaratibu mzima wa uchaguzi, na kuendeleza kushuka kwa demokrasia ya nchi, taarifa ya wizara ya mambo ya nje imesema.

Taarifa imesema imeisihi serikali ya Tanzania kubadili mwelekeo wake na kuwawajibisha waliohusika katika kuvuruga uchaguzi, manyanyaso na ghasia. Marekani itafuatilia kwa karibu sana maendeleo ya nchini Tanzania na haitasita kuchukua hatua za ziada dhidi ya waliohusika kudumaza demokrasia na kukiuka haki za binadamu.

Wagombea wa upinzani mara kwa mara walienguliwa na kunyanyaswa.

XS
SM
MD
LG