Operesheni hiyo ya usalama iliyowasilishwa rasmi leo kwa waziri wa mambo ya ndani Gerald Darmanin, itashuhudia mkusanyiko wa vikosi vya usalama mjini Paris, ambako umati mkubwa unatarajiwa iwapo Ufaransa itashinda.
Barabara ya Champs-Elysees ilikuwa eneo la sherehe kubwa wakati wa ushindi wa awali wa Ufaransa wa kombe la dunia mwaka wa 1998 na 2018, ambapo watu 600,000 walishangilia na kucheza muziki sehemu hiyo miaka minne iliyopita.
Barabara hiyo itafungwa Jumapili na maafisa 2,750 watakuwa karibu na eneo hilo.
Polisi watakuwa makini kukabiliana na watu wanaofanya vurugu, ni baada ya wafuasi 40 wa siasa kali za mrengo wa kulia kukamatwa Jumatano jioni walipojaribu kuungana na umati wa watu waliokuwa na furaha, baada ya Ufaransa kuishinda Morocco katika nusu fainali.