Amri ya kufukuzwa kazi kwa mkuu wa SBU Ivan Bakanov ambaye ni rafiki wa Zelenskiyy tangu utotoni, na mwendesha mashtaka mkuu Iryna Venediktova zilichapishwa kwenye tovuti rasmi ya rais muda mfupi baada ya hatua hiyo kuchukuliwa. Kupitia ujumbe tofauti wa Telegram, Zelenskyy amesema kwamba amechukua hatua hiyo baada ya kubainika kwamba baadhi ya maafisa kutoka idara za wakuu hao walikuwa wakishirikiana na Russia.
Ameongeza kusema kwamba jumla ya kesi 651 za usaliti na kushirikiana na Russia zimefunguliwa dhidi ya maafisa wa usalama, huku nyingine 60 zikiwa dhidi ya maafisa kutoka ofisi za Bakankov na Benediktova. Zelenskyy sasa ametangaza Oleksiy Symonenko kuwa mkuu mpya wa idara ya kuendesha mashitaka.