Taarifa ya kamandi kuu ya jeshi la Marekani CENTCOM, bila kutoa maelezo zaidi, imesema kwamba jeshi la Marekani limetekeleza operesheni iliyofanikiwa kwa kutumia helikopta mashariki mwa Syria saa nane dakika 57 usiku na kuwaua maafisa wawili wa ISIS.
Kati ya waliouawa ni Anas ambaye ni afisa wa Islamic state katika mkoa wa Syria, aliyesimamia operesheni za kundi hilo mashariki mwa Syria.
Kundi la haki za binadamu linalofuatilia vita vya Syria, limesema kwamba operesheni hiyo ndiyo kubwa zaidi kufanyika Syria katika muda wa wiki tatu zilizopita.
Mkuu wa kundi hilo la kufuatilia vita vya Syria Rai Abdel Rahman, amesema kwamba kitengo cha kupambana na ugaidi cha jeshi la Kikurdi la Syria, kimeshiriki katika operesheni hiyo katika Kijiji cha Al-Zor mashariki mwa mkoa wa Deir el-Zour.