Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 07, 2023 Local time: 15:31

Maafisa wa Marekani wanaonya kuhusu uwezo wa IS kuchochea ghasia


Alejandro Mayorkas, naibu waziri wa usalama wa ndani Marekani.
Alejandro Mayorkas, naibu waziri wa usalama wa ndani Marekani.

Maafisa wa Marekani wanaonya kuhusu uwezo wa kundi la Islamic State kuchochea mambo ya ghasia kote duniani ikiwemo nchini Marekani bila ya kuwa na uongozi au mawasiliano ya moja kwa moja na magaidi.

Naibu waziri wa usalama wa ndani wa Marekani, Alejandro Mayorkas aliliambia jopo la senate siku ya Alhamis kuwa wako katika awamu mpya ya vitisho vya ugaidi ulimwenguni na kuongezea tumeondoka katika mashambulizi ya moja wa moja ya kigaidi na kuingia katika dunia ambayo kuna ongezeko la mashambulizi yanayochochewa na ugaidi, moja ambayo mshambuliaji kamwe hajawahi kukutana ana kwa ana na mwanachama wa taasisi ya kigaidi lakini badala yake amehamasishwa na ujumbe na propaganda za ISIL.

Mdemocrat wa juu katika kamati ya usalama wa ndani kwenye senate amekubaliana na tathmini hiyo akielezea shambulizi la kigaidi la mwaka jana huko San Bernardino katika jimbo la California nchini Marekani ambalo lilisababisha vifo vya watu 14.

XS
SM
MD
LG