Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 14:20

Maafisa wa Algeria wawakamata ndugu wa mpinzani anayetafutwa


Mwanaharakati Amira Bouraoui akionyesha ishara ya ushindi baada ya kuachiliwa kutoka gereza ya Kolea, magharibi mwa Algiers, Julai 2, 2020.
Mwanaharakati Amira Bouraoui akionyesha ishara ya ushindi baada ya kuachiliwa kutoka gereza ya Kolea, magharibi mwa Algiers, Julai 2, 2020.

Mamlaka za Algeria zimemkamata mama na dada wa mwanaharakati anayetafutwa Amira Bouraoui siku chache baada ya mwanamke huyo kwenda Ufaransa, kundi la kutetea haki za binadamu na radio moja wamesema Jumapili.

. Bouraoui, daktari mfaransa mwenye asili ya Algeria, alikamatwa nchini Tunisia wiki iliyopita na alikabiliwa na hatari ya kupelekwa Algeria, lakini hatimaye aliweza kupanda ndege kuelekea Ufaransa siku ya Jumatatu jioni wiki iliyopita.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 46 alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela nchini Algeria mwezi Mei mwaka wa 2021“ kwa kuukashifu Uislamu” na kumtusi Rais.

Kuondoka kwake baada ya Ufaransa kuingilia kati, kulisababisha sakata la kidiplomasia kati ya Algiers na Paris, huku Algeria ikimwita balozi wake kutoka Ufaransa kwa mashauriano.

Jumamosi, maafisa mjini Algiers walimkamata mama yake Khadidja Bouraoui, mwenye umri wa miaka 71, na dada yake Wafa na kusaka nyumba yao, Kamati ya kitaifa ya uhuru wa wafungwa (CNLD) na radio M ziliripoti.

Mapema Jumapili, Wafa aliachiliwa lakini mamake Bouraoui aliwekwa kizuizini na kuhamishwa huko Annaba karibu na mpaka na Tunisia, CNLD imesema.

XS
SM
MD
LG