Vikosi vya usalama vya Israel vilisema wapiganaji wa Hamas walioshiriki katika shambulio la Oktoba 7 dhidi ya Israel wamekuwa wakitumia shule hiyo kama makazi yao na “kuelekeza ugaidi” kutoka kwenye shule hiyo.
Ofisi ya vyombo vya habari ya Hamas imetupilia mbali taarifa ya Israel na kusema wanajeshi wa Israel walitekeleza “uhalifu wa kikatili” dhidi ya watu waliokoseshwa makazi yao na kusema wanawake na watoto ni miongoni mwa waliofariki.
Msemaji wa jeshi la Israel Luteni Kanali Peter Lerner aliwambia waandishi wa habari kwamba Israel haikuwa na taarifa kuhusu vifo vya raia.
Shambulio hilo lilitokea kwenye shule inayosimamiwa na shirika la Umoja wa mataifa linalohudumia wakimbizi wa Palestina huko Nuseirat.
Kamishna mkuu wa shirika hilo la misaada la Umoja wa mataifa Philippe Lazzarini, amelielezea tukio hilo kama “ siku nyingine ya ukatili huko Gaza.”
Forum