Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 05:54

Maafisa sita wa Iran wawekewa vikwazo na Marekani


Marekani, Jumatano imewawekea vikwazo maafisa sita wa shirika la habari la serekali ya Iran.

Vikwazo vinatokana na kushiriki kwao katika kurusha taarifa za ushuhuda wa kulazimisha wa Wairan ambao ndugu zao wamefariki dunia wakiwa chini ya polisi.

Maafisa wa Marekani wamedai maafisa sita walirusha mahojiano ambayo ndugu wanadai wanafamilia wao waliuwawa na serekali ya Iran wakati wa maandamano ya miaka kadhaa ya nyuma.

Taarifa za vifo vyao zilibadilishwa na kudai walikufa kwa bahati mbaya na kwa sababu zisizo julikana.

Brian Nelson, wa kitengo cha ujasusi wa kigaidi na kifedha katika wizara ya fedha ya Marekani, amesema serekali ya Iran kwa kimkakati kabisa ililazimisha watu kutoa ushuhuda ambao ulidanganya wananchi na jumuiya ya kimataifa.

Nelson ameendelea kusema Marekani itaendelea kuwajibisha maafisa wa Iran na taasisi za serekali zinapo vunja haki za binadamu.

XS
SM
MD
LG