Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 30, 2023 Local time: 22:58

Maafisa polisi wa Ghana kukutana na jamii ya waislam


Mabango ya kampeni za uchaguzi huko Ghana.

Msemaji wa polisi wa Ghana, Cephas Arthur alisema maafisa wa polisi wanapanga kukutana na jamii ya waislam wiki hii kama sehemu ya juhudi za kukutana na washikadau wote ili kuhakikisha uchaguzi wa urais, wabunge na halmashauri za mji unafanyika kwa amani kama ulivyopangwa kufanyika Disemba saba mwaka 2016.

Msemaji huyo wa polisi pia alisema kuna washikadau wengine ambao wawakilishi wa polisi wanapanga kukutana kabla ya upigaji kura ujao. Hatua hii ni baada ya mkutano wa karibuni kati ya inspekta mkuu wa polisi wa Ghana, John Kudalor na baraza la maskofu wa kikatoliki katika mji mkuu wa jimbo la kaskazini wa Tamale.

Makundi ambayo polisi mpaka sasa wamekutana nayo ni kamisheni ya taifa ya vyombo vya habari, vyombo vya habari, baraza la amani la taifa, makundi mbali mbali ndani ya vyama vya kisiasa na baraza la wakristo wa Ghana. Arthur alisema polisi wameanzisha kampeni ya elimu nchi nzima wakitumia mtandao wa kijamii kuhusisha umma, kuhusiana na umuhimu wa kuhakikisha uchaguzi mkuu unakuwa wa amani.

XS
SM
MD
LG