Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 06, 2023 Local time: 08:29

Maadhinisho ya wachimba migodi waliouwawa Afrika kusini miaka 10 iliyopita yafanyika


Maadhimisho ya Marikana Afrika kusini
Maadhimisho ya Marikana Afrika kusini

Hali ya huzuni ilitanda Jumanne wakati wa mkusanyiko wa takriban watu 5,000  nchini Afrika kusini wakiadhimisha miaka 10 ya kile kinachojulikana kama mauaji ya Marikana, ambapo polisi waliwauwa wachimba madini  34 mwaka  2012, waliokuwa wakifanya maandamano.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP baadhi ya maneno yaliyoandikwa kwenye fulana zilizovaliwa na waliohudhuria ni pamoja na- Miaka 10 ya kumbukumbu. Wengi waliohudhuria walikuwa wachimba madini wanaodai kwamba haki haijapatikana hadi sasa wala kutimizwa kwa ahadi ya nyongeza za mishahara pamoja na kuimarishwa kwa hali ya mazingira ya kazi.

Maadhimisho hayo yalifanyika kwenye eneo la mlima karibu na migodi ya Marikana iliyo karibu na mji wa Rutensburg ambao uko takriban kilomita 112 kutoka Johannesburg. Wengi walivalia mavazi ya rangi ya kijani kibichi na nyeusi ikiwa ni rangi za muungano wa wachimba madini pamoja na wafanyakazi wa ujenzi, Afrika kusini, wakati usalama ukilindwa na kundi ndogo la polisi . Kiongozi wa muungano huo Joseph Mathunjwa wakati akihutubia waliohudhuria aliomba haki kwa wanafamilia wa wachimba madini waliouwawa miaka 10 iliyopita.

XS
SM
MD
LG