Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 05:29

M23 wasitisha mapigano, ADF waua watu 11 na kuteka nyara wengine kadhaa DRC


Wanajeshi wa FARDC wakishika doria katika msako dhidi ya kundi la waasi la ADF

Mashambulizi mapya yanayoaminika kutekelezwa na waasi wa Allied democratic forces ADF, yameua darzeni ya watu, katika mji wa Beni, Kivu kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Waasi wa ADF walishambulia kijiji cha Masambo na kuua watu 11 na kuteka nyara watu wengine wawili.

Afisa wa shirika lisilo la kiserikali Gilbert Kambale, amesema kwamba idadi ya watu waliouawa imefikia watu 15.

Wakaazi wa mji huo wameitisha maandamano dhidi ya serikali kulalamikia ukosefu wa usalama licha ya kuwepo idadi kubwa ya walinda usalama sehemu hiyo.

Wanaharakati wameitisha maandamano kulalamikia hatua ya kumfunga gerezani mmoja wa wanaharakati wa kundi la Lucha linalopigania mabadiliko nchini DRC, aliyekamatwa katika maandamano yaliyopita.

Kulingana na msemaji wa Polisi wa Beni Nasson Murara, watu 11 wamekamatwa mapema Jumatatu wakati wa maandamano.

XS
SM
MD
LG