Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 07, 2023 Local time: 15:59

M23 wapigana na jeshi la DRC


Waasi wa M23 wakati wakiondoka karibu na mji wa Sake, magharibi ya Goma, Novemba 30, 2012
Waasi wa M23 wakati wakiondoka karibu na mji wa Sake, magharibi ya Goma, Novemba 30, 2012
Mapigano mapya yamezuka huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kati ya jeshi la serikali na kundi la waasi wa M23, yakiwa ni mapambano ya kwanza kati ya pande hizo mbili baada ya takribani miezi sita.

Ripoti za awali zilisema pande hizo mbili zilipigana kwa saa kadhaa Jumatatu eneo la kaskazini mwa Goma.

Kundi la M23 lilisema jeshi lilivamia kituo kimoja cha waasi. Hakukuwa na matamshi ya haraka juu ya idadi ya vifo.

M23 iliuteka mji wa Goma mwezi Novemba kabla kundi hilo kuondoka kufuatia shinikizo kali la kimataifa. Mazungumzo ya amani yamekuwa yakifanyika kwa muda mrefu kati ya serikali na waasi na hivi sasa yamekwama.

Kikosi cha kwanza cha wanajeshi maalum wa Umoja wa mataifa kiliwasili Goma mwezi huu kwa ajili ya kazi zao za kupambana na waasi wa M23 pamoja na makundi mengine ya waasi.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa liliidhinisha tume ya ulinzi mwezi machi baada ya majaribio ya miaka kadhaa yaliyofanywa na serikali ya DRC kuleta uthabiti kwenye jimbo la Kivu kaskazini na majimbo ya jirani. Eneo hilo ni makazi ya makundi mengi ya waasi ambayo yanapigana juu ya eneo lenye utajiri wa madini.

Ripoti ya pamoja ya ofisi ya haki za binadamu katika Umoja wa mataifa mwezi huu iliwashutumu wote jeshi la DRC na kundi la m23 kwa kuhusika kwa ukiukaji wa haki za binadamu.

Ilisema mapambano ya pande zote yalisababisha kuwepo kwa wizi wa mali katika nyumba na raia kubakwa pamoja na ukatili mwingine.
XS
SM
MD
LG