Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 01:43

M23 wakubali kuondoka kwa taratibu maeneo wanayo shikilia DRC


Waasi wa M23 wamekubali kuendelea kuondoka kwa utaratibu kutoka katika eneo walilotekwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, rais wa zamani wa Kenya, Uhuru Kenyatta alisema Alhamisi. 

Kenyatta alikutana na viongozi wa M23 kwa nafasi yake kama mpatanishi katika mzozo huo kwa niaba ya jumuiya ya mataifa saba ya Afrika Mashariki, kulingana na taarifa kutoka ofisi yake.

Kundi la M23 linaloongozwa na watutsi limeteka maeneo mengi katika jimbo la Kivu Kaskazini katika miezi ya hivi karibuni na kuelekea mji mkuu wake Goma.

Lakini kutokana na shinikizo kali la kimataifa, iliahidi kuondoka huko na Ijumaa iliyopita na kuirudisha kambi muhimu ya jeshi la Kongo kilomita 40 kaskazini mwa Goma.

Katika kuonyesha nia njema na utayari wa kufanya kazi ili kusuluhisha hali ya Kivu Kaskazini, viongozi wa M23 walikubali kuendelea utaratibu wa kujiondoa na kuheshimu sitisho la mapigano," Kenyatta alisema katika taarifa hiyo baada ya mkutano huo katika mji wa pwani ya Kenya wa Mombasa.

“Walikubaliana zaidi kuendelea kuheshimu na kushirikiana na Jeshi la Kanda la Afrika Mashariki ambalo kwa sasa limeanza kudhibiti maeneo yaliyoachwa na M23,” aliongeza.

M23, ambao jina lake ni "The March 23 Movement", walishika tena silaha kupambana na serikali mwishoni mwa 2021, wakiishutumu Kinshasa kwa kushindwa kuheshimu ahadi za kuwajumuisha tena waasi katika jeshi.

XS
SM
MD
LG