Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 08:35

Watoto wa Lumumba kufungua mashitaka


Ramani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.
Ramani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Watoto wa Lumumba wasema watafungua mashitaka dhidi ya Wabelgiji wanaoshutumiwa kumuua.

Watoto wa kiongozi wa uhuru wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Patrice Lumumba, wanasema watafungua mashtaka ya uhalifu wa kivita dhidi ya raia 12 wa Ubelgiji wanaoshutumiwa kuhusika katika kifo cha baba yao, takribani miaka 50 iliyopita.

Guy Lumumba aliwaambia waandishi wa habari huko Brussels Jumanne, yeye na kaka zake watafungua mashtaka dhidi ya raia hao 12 katika mahakama moja ya Ubelgiji mwezi Oktoba.

Shirika la habari la AFP lilimkariri akisema Wabelgiji hao 12 wangali hai.

Mwanasheria huyo Christophe Marchand alikataa kutaja majina ya watuhumiwa lakini alisema watu hao wote walikuwa Congo wakati wa kifo cha Patrice Lumumba. Lumumba alikuwa kiongozi wa kwanza kuchaguliwa kwa njia ya kidemokrasia huko Congo, baada ya kupata uhuru kutoka Ubelgiji mwaka 1960.

XS
SM
MD
LG