Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 08:54

Lumumba asema lazima viongozi wawajibike kutokana na rushwa Kenya


Patrick Lumumba mkurugenzi wa KACC, tume ya kupambana na ulaji rushwa Kenya
Patrick Lumumba mkurugenzi wa KACC, tume ya kupambana na ulaji rushwa Kenya

Mkuu wa tume ya kupambana na rushwa Kenya PLO Lumumba atowa wito kwa viongozi kujiuzulu pindi kuna tuhuma katika wizara zao hata kama hawahusiki

Mkuu wa tume ya kupambana na rushwa Kenya, Patrick Lumumba alitowa wito wa kujiuzulu waziri wa elimu Sam Ongeri na katibu mkuu wake James Kiyiapi, kufutana na ripoti kwamba kiasi cha dola milioni 25 zimetumiwa vibaya katika wizara ya elimu kati ya mwaka 2005 na 2009.

Akizungumza na Sauti ya Amerika siku ya Jumatano, Bw. Lumumba alisema "kuna fedha zilizofujwa takriba Sh. bilioni 4.2 za Kenya kutoka wizara ya elimu baada ya baadhi ya watu kutowa amri na idhini kupitia kwa benki ya kwamba fedha zisafirishwe mpaka shule fulani. Na kuna shule zilizopokea fedha ambazo hazijulikani hazipo ni shule pepo."

Mkuu huyo wa kupambana na rushwa anasema wameshakamilisha upepelezi juu ya ufujaji fedha katika miaka ya nyuma na wamewafikisha maafisa 25 wa wizara ya elimi mahakamani.

XS
SM
MD
LG