Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 10:22

Libya:mapigano yaendelea Misrata


risasi nzito zikiwa zimepiga katika majengo ya misrata

Mapigano yalisikika katika mji ulozingirwa wa misrata nchini Libya

Mapigano yalisikika katika mji ulozingirwa wa misrata nchini Libya ambako majeshi ya serikali yameshutumiwa kutumia mabomu hatari yanayolipuka kwa mapande katika mapiagno yanayoendelea.

Msemaji wa waasi aliliambia shirika la habari la reuters kwamba majeshi yanayomtii kiongozi wa Libya moammar gadhafi yalifyatua takriban roket 100 katika mtaa wa viwanda kwenye mji huo jumamosi.

Amesema hakuna ripoti ya majeruhi.

Kundi la kutetea haki za binadamu human rights watch jana lilisema kuwa majeshi ya serikali yalitunmia mabomu yanayopasuka kwa mapande chungu nzima katika maeneo ya makazi na kusababisha hatari kubwa kwa wananchi.

XS
SM
MD
LG