Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 10:26

Upinzani Libya unatayarisha enzi mpya baada ya Ghadafi


Afisa wa jeshi la waasi anatowa mafunzo ya kutumia silaha kwa raia walojitolea kujiunga na jeshi la waasi mjini Benghazi, Mei 11, 2011
Afisa wa jeshi la waasi anatowa mafunzo ya kutumia silaha kwa raia walojitolea kujiunga na jeshi la waasi mjini Benghazi, Mei 11, 2011

Seneta John Kerry amesema wakati raia wa libya wanalindwa na ushirika wa NATO mpango unafanyika wa kutayarisha enzi baada ya Moammar Gadhafi.

Mwenyekiti wa kamati ya Seneti ya Marekani ya masula ya kigeni, Seneta John Kerry amesema wakati raia wa Libya wanalindwa na ushirika wa kijeshi unaoongozwa na NATO mpango unafanyika wa kutayarisha enzi baada ya Moammar Gadhafi.

Seneta Kerry alizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutana na kiongozi wa upinzani wa Baraza la Mpito la Taifa la Libya, Mahmoud Jabril, aliye ziarani Marekani.

Seneta huyo amesema awamu ya kwanza ya uvamizi wa jeshi la kimataifa huko Libya imefanikiwa."Tumefanikiwa katika jukumu la kwanza, ambalo lilikuwa ni kuzuia mauaji ya halaiki ya raia yanayofanywa na la Kanali Gadhafi nchini humo."

Mdemokrat huyo wa Massachusetts alisimama pamoja na kiongozi wa Mahmoud Jibril, baada ya kukutana nae katika afisi yake na akasema, ingawa hawajaweza kumuodowa Moammar Gadhafi bado lakini Baraza hilo linajiandaa kwa siku za baadae.

Kerry anasema baraza hilo la mpito la taifa limetayarisha mpango wa mfumo wa kidemekrasia nchini Libya baada ya gadhafi.Lakini anasema watahitaji msaadawa kila aina ili kufikia lengo hilo.

Anasema Kanali Gadhafi amedhibiti taasisi muhimu za serikali yake na jamii ya kiraia. Itabidi mfumo unoafanya kazi wa kidemokrasia kujenga upya taasisi hizo zote

Jibril kwa upande wake alifafanua zaidi maelezo ya Seneta kwa kusema kwamba "tangu siku ya kwanza ya upinzani wetu huko Libya tumedai kwamba ndoto yetu na muelekeo wetu ni kutayarisha katiba yenye misingi ya kidemokrasia, chini ya misingi ya haki za binadam na mashirika ya kiraia iliyo imara."

Hata hivyo Jabril alisema mahitaji ya walibya ni mengi na wanahitaji kila aina ya msaada utakaoweza kupatikana.

Na njia moja kufikia malengo hayo amesema Jibril, ni kuachiwa mali ya Ghadafi inayoshikiliwa na Marekani.

XS
SM
MD
LG