Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:22

Libya yatingishwa tena na mashambulizi ya anga huku falme za kiarabu zikiahidi misaada


Mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi mbalimbali wakipiga picha ya pamoja baada ya mkutano Abu Dhabi,
Mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi mbalimbali wakipiga picha ya pamoja baada ya mkutano Abu Dhabi,

NATO yashutumiwa kushambulia mji mkuu wa libya kwa kutumia ndege zake huku mataifa ya kiarabu yakiahidi msaada wa kifedha.

Mashambulizi mapya ya anga yanayodhaniwa kufanywa na NATO yametingisha mji mkuu wa Libya siku moja baada ya mataifa ya suhirika huo na mataifa ya kiarabu kuahidi zaidi ya dola bilioni 1.1 kusaidia baraza la upinzani la Libya na raia wanaoathiriwa na mzozo wa nchi hiyo.

Wajumbe 22 wa kundi la mawasiliano la Libya walitangaza orodha ya misaada ya fedha Alhamisi wakati wakikutana huko Umoja wa Falme za Kiarabu kutayarisha utawala mpya wa Libya bila kuwepo kiongozi Moammar Gadhafi.

Italy ambayo ni mtawala wa zamani wa Libya imesema itatoa msaada wa takriban dola milioni 600 kwa waasi wa Libya wakati Ufaransa imeahidi zaidi ya dola milioni 420 za msaada. Pia Kuwait, Qatar na Uturuki nazo zimeahidi msaada wa fedha.

Marekani haikupendekeza msaada moja kwa moja kwa waasi lakini ilitangaza msaada zaidi wenye thamani ya dola milioni 26.5 zaidkwa ajili ya huduma za kibinadamu kwa raia wa Libya.

Waziri wa mambo ya nje wa marekani Hillary Clinton aliuambia mkutano huo kuwa siku za bwana Gadhafi zimefikia mwisho. Baadae alieleza Baraza la mipto la Kitaifa la waasi kuwa mwakilishi halali wa watu wa Libya.

XS
SM
MD
LG