Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 11, 2023 Local time: 03:48

Majeshi yanayotii serikali mpya Libya yarudisha nyuma Islamic State


Majeshi yanayotii serikali mpya ya Libya.

Majeshi yanayounga mkono serikali mpya ya Libya yanaripotiwa kupata mafanikio ndani ya mji wa pwani unaoshikiliwa na kundi la Islamic State wa Sirte, wakati majeshi yanayounga mkono serikali pinzani huko Tobruk yanaeleza yamesukuma nyuma wapiganaji wa Alqaeda huko Benghazi.

Wanamgambo wanounga mkono serikali ya Umoja walikamata wilaya mbili ndani ya Sirte kati kati ya mapigano makali na kumekuwa na ripoti za majeruhi kwa pande zote mbili.

Ahmed Hadiya msemaji wa majeshi yanaounga mkono serikali huko Sirte aliiambia Televisheni ya Libya kwamba mapigano yalitokea katika maeneo kadhaa,

Anasema majeshi yanayounga mkono serikali yamewasukuma nyuma wapiganaji wa ISIS nje ya wilaya za Zafran na Gharbiyat na kuwabana katika maeneo madogo ya wilaya 700 na kituo cha mikutano cha Ouagadougou .

Wapiganji wa Islamic State waliripotiwa kupigana kwa bidii licha ya hasara waliyopata hivi karibuni , wakitumia mabomu ya kwenye gari, walipuaji mabomu wa kujitoa muhanga na mabomu ya kutegwa ardhini.

Kamanda wa jeshi la serikali huko Sirte aliwaambia waandishi wa habari kwamba wapiganji wa ISIS walikuwa na magari yaliojaa mabomu na wanajitahidi kuizuia serikali kuingia mjini.

Gazeti la Libya la Herald linaripoti kwamba wanamgambo 170 wanaounga mkono serikali wameuwawa na zaidi ya 700 wamejeruhiwa tangu kuanza kwa operesheni ya kijeshi iitwayo “Bunyan al Marsous” ili kukomboa Sirte.

Gazeti hilo limeeleza kwamba wapiganaji wengi majeruhi walipelekwa katika hospitali kuu ya Misrata ambako madaktari waliwakatalia waandishi wa habari kuchukua picha . Ilieleza kwamba wengi wa walioathirika wamepata majeraha makubwa na hali katika hospitali ilikuwa mbaya sana kwasababu ya ukosefu wa madawa ya antibiotics na pia manesi.

Vyombo vya habari vya Libya pia vimeripoti mapigano makali katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Libya wa Benghazi wakati majeshi yanayounga mkono serikali huko Tobruk yakipambana kuondoa wanamgambo wa kiislam wanaounga mkono al qaida.

Mapigano makali dhidi ya wanamgambo hao yalitokea katika mji wa Ajdabiya siku kadha zilizopita.

Msemaji wa vikosi vya Libya mashariki mwa nchi na mfuasi wa kamanda wa kijeshi Khalifa Haftar aliwaambia waandishi wa habari kwamba majeshi yake yanawashambulia wanamgambo karibu na wilaya za Sabari na Souq al Hout karibu na Benghazi.Jeshi la Libya limetoa madai kama hayo ya kuwasukuma nyuma wanamgambo huko Benghazi katika siku za nyuma.

Majeshi yanayomuunga mkono Jenerali Haftar pia yamefanya mashambulizi ya anga dhidi ya maeneo ya kundi la Islamic State karibu na Ajdabiya na eneo la mashariki ambalo ni ngome kuu ya wanamgambo ya Darna katika siku za karibuni.

XS
SM
MD
LG