Kukamatwa huko kunajiri baada ya raia mwingine wa Marekani, ambaye alikuwa akifundisha katika shule ya lugha katika mji mkuu Tripoli, kuzuiliwa kwa “kuwashawishi watoto wetu kuukana Uislamu na kubadili dini na kuwa Wakristo”.
Alhamisi, idara ya usalama wa ndani ilisema ilimkamata naibu mkurugenzi wa shule hiyo mjini Tripoli, ikimtambulisha kwa herufi za kwanza “SBO”.
Idara hiyo imemshutumu kwa kufanya kazi katika kampuni na mke wake kama mhubiri kwa niaba ya kanisa liitwalo Assemblies of God ili kuwapotosha watoto wa watu wetu Waislamu.
Kanisa la Assemblies of God lina makao yake katika jimbo la kusini mwa Marekani la Arkansas.