Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 04:21

Libya yaingia katika mazungumzo ya amani


Wabunge wa Libya.
Wabunge wa Libya.

Bunge la Libya, lililochaguliwa na wananchi limekubali kurudi katika majadiliano ya amani yanayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, hii ni wiki moja baada ya kujitoa na mjumbe wa Bunge linalohasimiana kusema mazungumzo yanatarajiwa kuanza siku ya Alhamisi.

Mataifa ya magharibi yanaona mazungumzo ya Umoja wa Mataifa kama nafasi pekee ya kumaliza mzozo wa Libya wa kugombania madaraka kati ya serekali mbili pinzani na majeshi yao.

Hali ya kutoelewana inaweza kuhatarisha kuipeleka nchi hiyo katika vita zaidi ya wenyewe kwa wenyewe inayokaribia miaka minne sasa tangu kuondolewa kwa utawala wa Muammar Gaddafi.

Wakati huo huo, Khalifa Haftar, kiongozi muhimu katika mapinduzi ya Libya amechaguliwa kuwa mkuu wa jeshi la serikali inayotambulika kimataifa.

Uteuzi wa Haftar unaonekana unaweza kuleta taharuki katika mazungumzo hayo ya Umoja wa Mataifa ya kujaribu kumaliza mzozo wa nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG