Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 30, 2023 Local time: 22:51

Libya yaahirisha uchaguzi wa bunge.


Maandamano ya wanajeshi Benghazi Libya .

Mkuu wa tume ya uchaguzi amesema uakhirishaji huo ulihitajika ili kuwapa wapiga kura muda wa kujiandikisha na kuangalia sifa za wagombea.

Libya imeahirisha uchaguzi wa kihistoria mpaka mwezi ujao ili kulipa taifa muda zaidi kujiandaa kwa kura hiyo ya kwanza tangu kuondolewa madarakani mwaka jana kwa kiongozi wa kidiktetea wa muda mrefu Moammar Gadhafi kufuatia uasi wa silaha.

Tume ya Umoja wa mataifa Libya ulisifu uamuzi wa kubadili tarehe ya uchaguzi wa bunge kutoka tarehe ya awali ya Juni 19 hadi July 7,ikisema itawezesha matayarisho muhimu kukamilishwa kabla ya kupiga kura. Katika taarifa iliyotolewa jumapili mwakilishi wa Umoja wa mataifa Ian Martin alisema tume ya taifa ya uchaguzi ya Libya imefanya maendeleo makubwa katika kile alichokiita ratiba yenye mamabo mengi na changamoto kubwa za utendaji kazi.”

Mkuu wa tume ya uchaguzi ya Libya Al-Abbar amesema uakhirishaji huo wa siku 18 ulihitajika ili kuwapa wapiga kura muda mrefu wa kujiandikisha na wahusika muda zaidi kuangalia sifa za wagombea . Akiongea kwenye mkutano wa waandishi wa habari mjini Tripoli amesema tume yake ilianza kazi Februari , ikiwa na muda mfupi kuandaa uchaguzi wa kwanza wa kitaifa kwa zaidi ya miongo minne.

XS
SM
MD
LG